Taarifa Kuhusu Vurugu za Baada ya Uchaguzi na Utumuzi Mbaya wa Mfumo wa Haki na Jinai.
Jopo hili limetambua kwa masikitiko kuhusu kuendelea kuzuiliwa kwa viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa kote nchini Tanzania.Taarifa za kukamatwa viongozi wengi wa upinzani Tanzania bara na Zanzibar ni ishara ya ukiukaji haki za kibinadamu na kuvunjwa mikataba ya kimataifa kuhusu haki nchini humo.