Kwa njia ya Barua pepe
2 October, 2020
Mwenyekiti,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,
P O Box 10923
Foreign Affairs Building, Shaaban Robert Str and Garden Avenue, Dar es
Salaam
uchaguzi@nec.go.tz
Mpendwa Jaji wa Rufaa Mstaafu Semistocles Kaijage,
KUH: Kuongezeka kwa visa vya uvunjivu wa amani kabla ya uchaguzi mkuu Tanzania.
Pokea salamu.
Jopo la Watu Mashuhuri wanaofuatilia uchaguzi wa Tanzania, kutoka Uganda, Kenya na Botswana linazidi kufuatilia matukio kwa karibu katika taifa hilo linapoelekea katika uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba mwaka wa 2020.
Huku jopo likipongeza maandalizi yaliyowekwa na tume ya taifa ya uchaguzi katika kufanikisha uchaguzi wa amani, tungependa kukufahamisha kuhusu masuala ibuka
yafuatayo.
1. Kuongezeka kwa visa vya uvunjivu wa amani kabla ya uchaguzi
Katika muda wa wiki moja iliyopita, visa vilivyohusisha vyama vya kisiasa, umma na vyombo vya dola vimeripotiwa kwenye maeneo kadhaa ya taifa. Baadhi ya matukio makuu ya ghasia ni yafuatayo:
a. Mnamo tarehe 18 Septemba 2020, Chadema kiliripoti kutekwa nyara mgombea wake wa kiti cha udiwani wa wadi ya Kibosho, jimbo la Moshi Vijijini, , Gallus Chuwa na kulazimishwa kutangaza kujiondoa kaitka kinyanganyiro hicho.
b. Tarehe19 Septemba 2020, Simon Mwacha, mmoja wa viongozi wa Chadema katika kata ya Rundugai, jimbo la Hai, alishambuliwa kwa mapanga na watu waliodaiwa kuwa wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM);
c. Katika jimbo la Vunjo, Mkoa wa Kilimanjaro, wagombeaji udiwani walidaiwa kuvamiwa na kushurutishwa kujiunga na CCM.
d. Huko huko Vunjo, mnano tarehe 20 Septemba 2020, kiongozi wa chama cha NCCR Mageuzi na mgombeaji kiti cha ubunge James Mbatia aliripoti kuhusu kisa cha rafiki yake Deo Mosha kushambuliwa na kukatwa sikio;
e. Huko Zanzibar vijana wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CCM wakishirikiana na polisi walivamia ofisi za chama cha ACT Wazalendo tawi la Tutani (Mkombozi) Barza Nuur huko Nungwi na kuchana bendera za ACT-Wazalendo kabla ya kuweka za CCM. Tukio hilo liliripotiwa kaitka kituo cha polisi cha Nungwi;
f. Huko Arusha, Chadema kililalamika kuhusu baadhi ya mabango yake ya kampeni na magari kushambuliwa na watu waliodaiwa kuwa wafuasi wa CCM;
g. Huko Bukoba, Mkoa wa Kagera, tukio lililonaswa kwenye kanda ya video
linawaonyesha wafuasi wa CCM wakimrushia mawe mgombea urais wa Chadema Tundu Lissu alpohudhuria mkutano wa hadhara kaitka uwanja wa Gymkhana;
h. Huko Pemba, wilaya ya Wete, CCM kiliripoti kuwa wafuasi wake wawili , Khamis Nyange (Profesa Gogo) na Bakari Ali, walishambuliwa kwa mapanga kaitka msikiti wa Kangagi na watu waliotajwa kuwa wafuasi wa ACT-Wazalendo walipokuwa wakisali;
i. Katika mkoa wa Kilimanjaro, Mkuu wa Mkoa Mama Anna Mghwira, alionya kuhusu kuongezeka visa vya vurugu. Visa hivyo vilijumuisha kutekwa nyara na kushambuliwa na kutupwa katika misitu na mito.
j. Mnamo tarehe 24 Septemba, mkurugenzi wa mawasiliano wa chama cha CUF Abdul Kambaya alinukuliwa akilalamikia kuraruliwa bendera za chama hicho katika maeneo bunge kadhaa.
k. ACT-Wazalendo kimeripoti kuhusu visa vya watu kupigwa na kudhulumiwa na maafisa wa kikosi maalum cha walinda usalama vya Zanzibar (Vikosi vya SMZ) huko Pemba; na ,
l. ACT-Wazalendo pia kimeripoti kuwa polisi wanawazuilia maafisa wake watatu – Dotto Rangimoto, Dahlia Majid na Arodia Peter kufuata uvamizi katika makao makuu ya chama hicho eneo la Magomeni tarehe 25 Septema.
Visa hivi vya vurugu sharti vidhibitiwe mapema kabla ya kuchochea machafuko wakati uchaguzi ukikaribia. Tunavisihi vyama vya kisiasa, vyombo vya usalama na rais kufanya iwezekanavyo ili kuepusha vurugu zaidi huku pia tukiitaka tume ya uchaguzi kutoa onyo kali
kwa wanaohusika katika vurugu.
2. Kupigwa marufuku wagombeaji na usikizwaji wa rufaa zao.
Jopo hili aidha linasikitishwa na jinsi malalamishi ya baadhi ya wagombea waliopigwa marufuku yalivyoshughulikiwa. Tunaisihi tume ya uchaguzi kuzingatia haki na uwazi katika kusikiza na kutoa maamuzi kuhusiana na malalamishi hayo.
Tunafahamu kuwa baadhi ya malalamishi ya wagombeaji wa upinzani hayajasikizwa na kuamuliwa. Licha ya NEC kutangaza tarehe 18 Septemba kuwa ilikamilisha usikilizwaji wa malalamishi hayo. Aidha tunafahamu kuwa vyama vya; Chadema na ACT-Wazalendo havijaridhishwa na mchakato wa kusikiliza malalamishi hayo. Kwa mfano chama cha
Chadema kinadai kuwa malalamishi ya wagombea 16 wa ubunge na 300 wa udiwani hayajasikilizwa. Muasuala haya yanatishia uwezo wa NEC kuandaa uchaguzi wa kuaminika mwezi Oktoba.
3. Vikwazo vya kisheria
Jopo hili pia limegundua kutokuwepo ukosefu wa suluhusu za kisheria katika baadhi ya maamuzi ya vyombo vya usimamizi wa uchaguzi (EMB) inavyohitajika kikatiba, pamoja na kanuni za uchaguzi za mwaka 2020. Kwa mtazamo wetu, mapungufu ya kisheria yanahujumu uhuru wa wagombeaji kusaka haki kuhusiana na migogoro ya uchaguzi.
Kwa kuzingatia hili jopo linapendekeza kuwa:
- Tume za uchaguzi NEC na ZEC, pamoja na wadau wengine katika uchaguzi huu wazingatie amani, uadilifu na uwazi katika utendakazi wao.
- Vyama vya kisiasa, vyombo vya dola na umma vikome kuhusika katika vitendo vinavyohujumu amani na usalama wakati wa kampeni.
- Tume ya uchaguzi ichapishe sababu za kuwapiga marufuku wagombea.
Wako Mpendwa,
Prof. Frederick Ssempebwa
Mwenyekiti
Dr. Willy Mutunga
Wenyeviti wenza
Ms. Alice Mwonge
Wenyeviti wenza
Cc:
Jaji Francis S. Mutungi- Msajili wa vyama vya kisiasa
Bw. Simon Sirro- Inspekta Jenerali wa Polisi
Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu-Tume ya haki za binadamu (CHRAGG)
Vyama vya kisiasa
Vyombo vya habari
8 Comments
Rubben stephen
Safi sana ccm walibweteka sana kwamba watashinda ushindi wamezani sasa wataisoma namba mwaka huu nilazima waondoke wakapumzike
Rubben stephen
Nimewakubali
Paschal
Ni sahihi kabsa kwa vyombo vya kimataifa kufuatiilia mlolongo huu wa uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi uwe wa Amani,
Ahsanteni sana
Fenrick
Taarifa zenu very biased , sioni taarifa ya majuzi kule Njombe kiongozi wa CCM vyuo vikuu aliuawa na nyie mnakaa kimya kama activist, I expected you could have said something.
Yusuph
Is good!
You could send copy to ICC!
Is good because I think they will get customers from this election!
Haji Chang'a
Hii ni taarifa muhimu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu tarehe 28 October 2020.
Black
Tume inaonesha upendeleo wa Wazi kwa wagombea Wa ngazi zote za uchaguzi.
Mfano mgombea CCM akiwa Tunduma Alisema ” mkichagua hao wengine msitegeemee kuwaletaea mmi Maji, sitawaletea Maji” sasa hii haoneshi kuwa Ni kiongozi anaheshimu usawa wa maendeleo.
Andrew Kayanda
The days of ccm are numbered. October 28 is just around the corner and we Tanzanian are going to make a big historic change. Nobody / nothing can stop us.
FREEDOM IS COMMING TOMMOROW!!!