22 Septemba, 2020
Mwenyekiti,
Tume ya Uchaguzi Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
SLP 10923
Foreign Affairs Building, Shaaban Robert Street and Garden Avenue,
Dar es Salaam
uchaguzi@nec.go.tz
Kwa,
Jaji wa Rufaa (Mst) Semistocles Kaijage,
KUH: Jopo la Watu Mashuhuri la Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu Tanzania (TEW) Kuhusu Changamoto za Kisheria Katika Kuandaa Uchaguzi wa Huru na Haki Tanzania
Salamu kutoka kwa TEW.
Tanzania Elections Watch (TEW) ni mpango wa kikanda ambao jukumu lake ni kuangazia muktadha wa uchaguzi wa Tanzania na kutoa usuluhisho wa kikanda kwenye masuala hayo. Mpango huu unatokana na kuongezeka kwa ufuatiliaji wa kikanda na kimataifa kwenye masuala ya uchaguzi nchini Tanzania.
Mpango wa TEW umeleta pamoja jopo la watu mashuhuri inayojumuisha watu wenye ubobezi kutoka katika ukanda huu ili kujadili kwa kina maendeleo na mchakato wa uchaguzi mkuu kadri unavyochipuka ili kuhakikisha masuala ibuka yanajadiliwa kwa haraka hasusan mausla ya
ukiukwaji wa haki za binadamu a masuala ya kisiasa tukielekea uchaguzi mkuu 28 Oktoba 2020. Jopo hili liko chini ya uongozi wa wenyeviti wenza Prof. Frederick Ssempebwa Kutoka Uganda, Dkt. Willy Mutunga kutoka Kenya Na Bi. Alice Mogwe kutoka Botswana.
Jopo hili linatambua kuwa Tume ya Uchaguzi (NEC) mnamo tarehe 5 Juni 2020, ilichapisha Kanuni mbili za uchaguzi ambazo ni, Kanuni kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa(uchaguzi wa madiwani) ya mwaka 2020 pamoja na Kanuni ya uchaguzi mkuu (uchaguzi wa rais na ubunge) ya mwaka Uchapishaji wa kanuni hizi ni katika kutimiza majukumu ya tume ya uchaguzi NEC kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi mkuu (kifungu cha 343). Jopo hili pia linatambua hatua ya kuidhinishwa sheria ya mwaka 2018 ya uchaguzi ya Zanzibar iliyopelekea marakebisho ya sheria ya awali.
Jopo hili linatambua juhudi ambazo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeendelea kuweka kuandaa uchaguzi huru, wa haki na kuaminika kwa mujibu wa sheria za nchi na matakwa ya sheria za kimataifa. Licha ya jitihada za NEC na tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuendelea kujiandaa kwa uchaguzi, jopo hili limegundua mapungufu kadhaa na utata katika vipengele vya sheria na kanuni za uchaguzi, vikiwemo utekelezaji na muingiliano na katiba pamoja na sheria za kikanda na kimataitaifa.
Kwanza jopo hili linatambua malalamishi kutoka kwa mashirika ya kijamii na vyama vya kisiasa ya kutohusishwa kwa wadau katika kuandaa na kuidhinishwa kwa kanuni hizo mnano mwezi Juni, Tume ya uchaguzi inahitajiwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi kushauriana kwa kina na
wadau husika vikiwemo vyama vya kisiasa.
Pili, tunaipongezaTume kwa kuwaalika na kuwaidhinisha waangalilizi wa ndani na wa kimataifa kwa mujibu wa kipengele cha 18 cha Kanuni za uchaguzi nchini humo. Mualiko na kushiriki kwa waangalizi hao ni hatua muhimu katika kuhakikisha maandalizi ya uchaguzi huru wa wazi na haki.
Jopo hili linatambua kuhusu tangazo la NEC Tarehe 23 Juni 2020 la kuorodheshwa mashirika 96 kuwa waangalizi katika uchaguzi pamoja na kuidhinkishwa kwa waangalizi 17 katika uchguzi wa Zanzibar. Tunaipongeza NEC pia kwa kuwaalika na kuwaidhinisha waangalizi 15 wa kimataifa kama ilivyotangazwa na wizara ya mambo ya nje.
Jopo hili hata hivyo limesikitishwa na hatua ya NEC kuyanyima baadhi ya mashirika ya haki za kibinadamu nchini nafasi ya uangalizi wa uchaguzi huu nchini zikiwemo Kituo cha Sheria na haki za kibinadamu nchini humo (LHRC), shirika la Watetezi la THRDC na Jukwaa la Katiba. Jopo hili
pia linatambua pia kwamba Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) limenyimwa nafasi ya kuangalia uchaguzi huu. Jopo pia linatambua kwamba kunyimwa kwa nafasi hizi za uangalizi hakukuwa wazi
na hakuna maelezo yoyote yaliyotolewa mpaka sasa kwa maamuzi hayo ya Tume. Tungependa kuipongeza Tume kwa kuwaruhusu waangalizi kufuatilia uchaguzi huu kwa mujibu na matakwa ya kanuni za kimataifa. Hata hivyo azma hiyo njema ya Tume inatiwa doa na hatua
ya kuwepo vipengele vyenye utata katika sheria ya uchagizi mkuu. Kwa mfano misingi ya kipengele cha 22 cha sheria hizi kinahujumu madhumuni ya uangalizi wa ya uchaguzi. Matakwa haya yanakiuka uhuru wa umma kujieleza au kupata maelezo na yanakwenda kinyume na sehemu ya 6 ya kanuni za SADC kuhusiana na maandalizi ya uchaguzi wa kidemokrasia.
Nne, Jopo hili limeangazia vipengele vya Katiba, na kubaini kuwepo mkinzano kati ya Kanuni za uchaguzi na katiba ya Tanzania katika maandalizi ya uchaguzi wa ubunge. Kipengele cha 66(1)(B) cha katiba kinaelezea kuwa mbunge anastahiki kuchaguliwa ili kuwakilisha jimbo. Licha ya uchaguzi wa wabunge kuelekezwa kwenye katiba, kanuni ya uchaguzi inakinzana na katiba. Sheria ya Uchaguzi inafafanua kuwa mbunge anayeteuliwa bila kupingwa atatambulika kama mbunge aliyechaguliwa rasmi chini ya kipengele 28 cha sheria ya uchaguzi.
Mwisho, tathmini yetu kuhusu mchakato mzima wa sheria za uchaguzi umeainisha ukweli kuhusu mapungufu katika sheria ya uchaguzi. Mifano hai ni:
(a) Kipengele 41(7) katika katiba inazuia mahakama kuchunguza na kusikiza kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais. Hii ni kinyume na maamuzi na maelekezo ya hivi karibuni ya mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu katika kesi ya Jebra Kambole vs Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inayolaani uwepo wa kipengele hicho kwa kutotoa haki ya kusikilizwa kwa majibu wa mkataba wa haki za binadamu.
(b) Kipengele 39(7) cha sheria ya uchaguzi mkuu kinaeleza kuwa uamuzi wa tume chini ya sehemu ya (6) hauwezi kupingwa mahakamani. Jambo hilo linakiuka ibara ya 107 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977.
(c) Kipengele 143 cha sheria ya uchaguzi kinachoipa tume ya uchaguzi ya Zanzibar mamlaka ya kufanya mamuzi ya mwisho kuhusu uchaguzi mkuu na kuzuia mahakama kuwajibisha tume katika utekelezaji wa maamuzi yake. Jambo hilo linakinzana na mamlaka ya mahakama kuamua
haki kwa mujibu wa katiba na mikataba ya kimataifa.
Jopo hii linatoa wito kwa mamlaka husika hususan tume za uchaguzi za taifa (NEC) na ya Zanzibar (ZEC) kuzingatia matakwa ya kikatiba katika kuhakikisha mchakato huru na wa kuaminika wa maandalizi ya uchaguzi mkuu wa Tanzania.
Wako Mwaminifu
Prof. Frederick Ssempebwa -Mwenyekiti
Ms. Alice Mogwe – Naibu Mwenyekiti
Dr. Willy Mutunga – Naibu Mwenyekiti