Nairobi, Kampala, Gaborone, London 11 September 2020: Kundi la watu mashuhuri likiongozwa na wenye-kiti wenza watatu: Prof.Frederick Ssempebwa ( Uganda), Dkt.Willy Mutunga (Kenya) na Bi. Alice Mogwe (Botswana), linafuatilia kwa karibu hali nchini Tanzania kabla ya uchaguzi mkuu utakaoandaliwa tarehe 28 mwezi Oktoba mwaka, 2020. Wenyekiti hao wanawapongeza raia wa Tanzania kwa kuandaa chaguzi za kidemokrasia tangu kurejea siasa za vyama vingi mwaka wa 1995. Tunatoa wito kwa washika dau wote waendelee kuzingatia demokrasia na uongozi bora kupitia kuhakikisha kuwepo taasisi zenye uwazi, uwajibikaji na zinazoheshimu demokrasia kwa mujibu wa maafikiano ya kimataifa yakiwemo kanuni za shirika la SADC na mwongozo kuhusu uandalizi wa uchaguzi wa kidemokrasia.
Kundi hili linafahamu kuhusu taarifa iliyotolewa na tume ya uchaguzi tarehe 1 Septemba mwaka wa 2020 ikiwataka wagombeaji wote kuzingatia sheria namasharti ya uandaaji uchaguzi. Katika taarifa hiyo , tume hiyo ilidokeza kuangazia upya jumla ya malalamishi 557 kuhusiana na uchaguzi wa ubunge na viti vya baraza la wadi. Tunafahamu pia kuwa wakati wa usikizwaji malalamishi hayo, tume hii inapaswa kufuata kanuni za usimamizi wa haki. Jopo hili linafahamu kuhusu taarifa ya NEC ya tarehe 8, 9 na 11 mwezi septemba katika kutimiza wajibu wake, kwa kuambatana na kipengee 40(6) cha sheria ya uchaguzi sehemu ya 343. Tumetamaushwa kugundua kuwa malalamishi yote yanayodaiwa kuwasilishwa, ni ya wagombeaji kutoka vyama vya upinzani,kama ilivyodokezwa na viongozi wa kidini nchini humo.
Tungependa kusisitiza kuwa tume ya uchaguzi NEC haikuandaa vikao vya kusikiza malalamishi hayo kwa njia ya haki na usawa. Mianya katika kutekeleza uwazi, haki ya kusikika na kuhusishwa wagombeaji wote katika utoaji maamuzi kunatilia shaka uwezo wa NEC kuhakikisha haki imetendeka, hii ikiwa ni kati ya mengine katika kipengee 25 cha ICCPR.
Jopo limesikitishwa pakubwa na hatua ya kuwapiga marufuku makumi ya wagombeaji kutoka vyama vya upinzani ikiwemo katika kisiwa cha pemba na kuhujumu amani na uthabiti katika kisiwa hicho.kukosekana uwazi katika usikizwaji malalamishi hayo kunalitia hofu jopo hili kuhusu uwezo wa kuimarishwa kanuni za usawa kwenye uchaguzi.
Tumebaini kuwa thuluthi tano pekee ya malalamishi yamesikizwa kufikia sasa wakati kampeni za uchaguzi zikiendelea. Tunahofu kutokana na hatua ya NEC kuwatangaza washindi pasi na kupigwa baadhi ya wagombeaji mnamo tarehe 28 Agosti 2020 kinyume na kipengee cha 66 cha katiba ya Tanzania. Hatua ya NEC imewanyima raia wa Tanzania nafasi ya kutekeleza haki yao chini ya vipengee vya 5 na 21 vua katiba kuwachagua viongozi wao.
Jopo hili linatoa wito kwa tume ya kitaifa ya uchaguzi NEC na tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC kusikiliza billa upendeleo malalamishi yote yaliyosalia kutoka wagombeaji waliopigwa marufuku. Tunazisihi mamlaka za uchaguzi kuzingatia kanuni za usimamizi wa haki na kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuhujumu maandalizi ya uchaguzi wa kuaminika. Jopo la watu maalum linaendelea kufuatilia uchaguzi na kampeni za kisiasa na kusisitiza kujitolea kwetu kuwasaidia raia wa Tanzania kujiandaa vyema kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
One Comment
Emanuel Bitariho
Nec na zec ni matawi ya chama tawala ccm tungu mwaka 1995 wananchi watanzania wamekuwa hawasikilizwi wala kuhusisha kwenye maamuzi ya msitakabali wa maisha yao ndio maana tangu tupate uhuru umasikini tumezidi kuongezeka japo nchi wahisani zimekuwa zikitowa misada mingi ya kusaidia maendeleo. kwasababu viogozi wanajuwa wananchi hawana cha kuwafanya wamekuwa walitumia kodi na misaada kujinufaisha wenyewe. sasa mwaka huu tunaomba nchi zoto duniani zenye mapenzi mema na tanzania na Africa kwa ujumla zishinikize kuwepo kwa uchaguzi huru na haki. kinyume na hilo Tanzania itengwe na jumuiya zote za kimataifa. bila hivyo Tanzania itakwenda kuingia kwenye machafuko ya kisiasa kitu ambacho kitayumbisha mtengamano wa kisiasa na kiuchumi katika ukanda mzima wa Africa mashariki na kati. umoja wa Africa huu ni wakati kujijengea heshima kwa kuhakikisha katiba za nchi zote za kiafrica zinaheshimiwa na serikali.