Jopo hili linatambua kuwa Tume ya Uchaguzi (NEC) mnamo tarehe 5 Juni 2020, ilichapisha Kanuni mbili za uchaguzi ambazo ni, Kanuni kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa (uchaguzi wa madiwani) ya mwaka 2020 pamoja na Kanuni ya uchaguzi mkuu (uchaguzi wa rais na ubunge) ya mwaka Uchapishaji wa kanuni hizi ni katika kutimiza majukumu ya tume ya uchaguzi NEC kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi mkuu (kifungu cha 343). Jopo hili pia linatambua hatua ya kuidhinishwa sheria ya mwaka 2018 ya uchaguzi ya Zanzibar iliyopelekea marakebisho ya sheria ya awali.